# Maelezo ya Jumla Mwanamke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake. # Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu Kama mpenzi angekuwa kaka yake, angemleta kwa nyumba ya familia. Hii ilikuwa kawaida katika huo utamaduni na bado unaendelea kwa baadhi. # na utanifundisha Hii yaweza tafsiriwa kama "na ata nifundisha." Kwasababu mwanamke hana uzoefu wa kufanya mapenzi, ana fikiri kuwa mpenzi wake au mama yake angemfundisha jinsi ya kufanya mapenzi. # Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga Mwanamke anatumia haya maumbo kusema kuwa atajitolea kwa mpenzi wake na kufanya mapenzi naye. # mvinyo ulio chachwa "mvinyo wenye viungo" au "mvinyo wenye viungo ndani yake" Hii ya wakilisha nguvu ya kulevya ya mapenzi. # jwisi ya komamanga Mwanamke ana wakilisha kimiminika chake na maji ya komamanga. # Mkono wake wa kushoto...wanikumbatia Tazama ilivyo tafsiriwa "Mkono wake wa kushoto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia" ndani ya 2:5.