# Maelezo ya Jumla Mpenzi anaendelea kumsifu mwanamke. # Wewe ni bustani ya chemchemi "Wewe ni chemchemi katika bustani." Mpenzi ana elezea jinsi alivyo mzuri kwa kumfananisha na maji. # maji safi maji safi ya kunywa # mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni Kwasababu Lebanoni ilikuwa na milima iliyo funikwa kwa miti, mifereji kutoka Lebanoni ilikuwa misafi na ya baridi. # Amka ... manukato yake yatoe marashi Mwanamke anazungumza na upepo wa kaskazini na wa kusini kama ni watu. # Amka "Anza kwenda" # vuma katika bustani yangu Mwanamke ana utaja mwili wake kwa kuuongelea kama bsutani. # ili manukato yake yatoe marashi "itume harufu yake nzuri" # Mpenzi wangu na ... matunda ya chaguo Mwanamke anamkaribisha mpenzi wake kumfurahia kama mkewe. # matunda ya chaguo "matunda mazuri"