# Mimi ni mweusi lakini mzuri "Ngozi yangu ni nyeusi, lakini bado ni mzuri" # mweusi kama hema za Kedari Makabila ya kuhama hama ya Kedari yalitumia ngozi nyeusi ya mbuzi kujenga nyumba zao. Mwanamke analinganisha ngozi yake na hizi hema. # mzuri kama mapazia ya Sulemani Ana fananisha ngozi yake na mapazia mazuri Sulemani aliyo tengeneza ama kwa jumba lake au kwa ajili ya Hekalu. # limeniunguza "kuchomwa" # Wana wa mama yangu "Kaka zangu wa kambo." Hawa kaka zake labda walikuwa na mama mmoja kama huyu mwanamke lakini sie baba mmoja. # mtunzi wa mashamba ya mizabibu "mtu aliye tunza shamba la mizabibu" # lakini shamba langu la mizabibu sijatunza Mwanamke ana jilinganisha na shamba la mizabibu. "lakini sijaweza kujitunza mwenyewe."