# Lakini ikiwa ni kwa neema Paulo anaendelea kuelezea namna neema ya Mungu inavyofanya kazi. "kwa kuwa neema ya Mungu inafanya kazi kwa rehema" # Ni nini basi? "Tuhitimishe vipi?" "hivi ndivyo ambavyo tunapaswa kukumbuka." # Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie Huu ni ufafanuzi kuhusu ukweli kwamba niwabutu kiroho. Hawana uwezo wa kuona na kusikia ukweli wa kiroho. # Roho ya Hapa inamaanisha "kuwa na tabia za" mfano "roho ya hekima." # Macho ili wasione Kuona kwa jicho moja ilichukuliwa kuwa sawa na kupata uelewa. # Masikio ili wasisikie Kusikia kwa masikio ilichukuliwa kuwa sawa na utii.