# Sentensi unganishi: Paul anaeleza kuhusiana na shauku yake kwamba watu wa taifa la Israeli wangeokolewa, kisha anasisitiza njia tofauti ambazo Mungu ameandaa kwa kuamini. # na dhamiri yangu hushuhudia ndani yangu katika Roho Mtakatifu. Njia mbadala ya utofasiri: "Roho Mtakatifu huongoza dhamiri yangu na kuhakiki nisemacho" # kwa kuwa kwangu mimi kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu. Kama nafsi ya Paul ambayo inahuzunika inahitajika kusemwa, tumia tofasiri nyingine: " Ninakuambia kwamba ninahuzunika kwa wingi na kwa undani." # huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma Hii misemo miwili inamaanisha haswa maana ile ile. Paulo anatumia kwa pamoja kwa kusisitiza ni kwa namna gani hisia zake zilivyo.