# Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu "Kwa watu wote ambao Roho wa Mungu anawaongoza" # wana wa Mungu Hapa hii inamaanisha walioamini wote katika Yesu na mara nyingi hutafsiriwa kama "watoto wa Mungu." # Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa tena hata muogope "Kwa kuwa Mungu hakuwapa ninyi roho inayowanya ninyi kuwa watumwa tena wa nguvu ya dhambi na hofu ya hukumu ya Mungu" # ambayo kwayo tunalia "inayotufanya sisi tulie" # Abba, Baba "Abba" ni "Baba" kwa lugha ya Kiaramaiki.