# Kwa kuwa Paulo anaelezea namna ambavyo Mungu alijidhihirisha mwenyewe kwa wanabamu # Mambo yake yasiyoonekana yameonekana wazi "mambo yasiyoonekana" ni mambo yasiyoonekana kwa macho. Yamekuwa "yameonekana wazi" kwa sababu watu wameelewa kuwa wako pale japokuwa hawawezi kuona kwa macho yao. # Ulimwengu Hii inamaanisha mbingu na dunia, pamoja na vyote vilivyomo. # Asili ya Mungu "Ubora na tabia za Mungu" au "mambo ya Mungu yanayomfanya awe Mungu" # Wanaelewe kupitia vitu vilivyoumbwa "watu wanaweza kuelewa kuhusu Mungu kwa kuangalia vitu alivyovifanya" # Watu hawa hawatakuwa na udhuru "Watu hawa hawatasema kuwa hawakujua" # Wakawa wajinga kwenye mawazo yao "wakaanza kuwaza mambo ya kijinga" # Mioyo yao isiyo na hisia ilikuwa na giza Maelezo haya yanaonyesha moyo uliokuwa na giza ikimaanisha wamekosa uelewa. "mioyo yao haiwezi tena kuelewa"