# Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu atamuachia Shetani kutoka katika gereza lake" # kona nne za dunia Hii ni lugha inayomaanisha "duniani kote" # Gogu na Magogu Haya ni majina ambayo nabii Hezekia alitumia kuwakilisha mataifa ya mbali. # Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari Huu ni msisitizo wa namba kubwa sana la askari wa jeshi la Shetani.