# Taarifa ya Jumla: Hapa ni mwanzo wa maono mengine. Yohana anaanza kuelezea mpandaji wa farasi nyeupe. # Kisha niliona mbingu zimefunguka Hii picha inatumika kuashiria mwanzo wa maono mapya. # yule aliyekuwa amempanda Aliyempanda ni Yesu. # Huhukumu kwa haki Hapa "haki" inamaanisha kile kilicho sahihi. "Anahukumu watu wote kulingana na kile kilicho sahihi" # Macho yake ni kama mwali wa moto Yohana anazungumzia macho ya mpandaji kama vile yaling'aa kama mwali wa moto. # jina lililoandikwa juu yake Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu ameandika jina juu yake" # asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe "Yeye tu ndiye ajuae maana ya jina hilo" # Amevaa vazi lililochovywa katika damu Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Damu imefunika vazi lake" # jina lake anaitwa Neno la Mungu Unaweza kueleza hii kwa hali ya kutenda. "jina lake pia ni Neno la Mungu"