# akamwaga kutoka kwenye bakuli lake Neno "bakuli" linamaanisha kile kilichomo. "kumwagwa divai kutoka katika bakuli lake" au " kumwaga ghadhabu ya Mungu kutoka katika bakuli lake" # kiti cha enzi cha mnyama Hapa ndipo mnyama anapotawalia. Inaweza kumaanisha mji mkuu wa ufalme wake. # giza likaufunika ufalme wake Giza linazungumziwa kama vile ni kitu kama blangeti. "ikawa giza katika ufalme wake wote" au " ufalme wake wote ukawa giza" # Walisaga ... Wakamtukana Hapa inamaanisha watu katika ufalme wa mnyama.