# Taarifa ya Jumla: Huu mstari ni mapumziko kutoka katika hesabu ya maono ya Yohana. Hapa anawapa onyo jingine wasomaji wa hesabu yake. # Hii inahitaji busara "Hekima inahitajika" au "Unahitaji kuwa na busara kuhusu hili" # Ikiwa yeyote ana ufahamu Neno "ufahamu" inaweza kutafsiriwa na kitenzi "kuelewa." "Kama yeyote anaweza kuelewa vitu hivi" # mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama "Anapaswa kutambua maana ya namba ya mnyama" au "anatakiwa kujua maana ya namba ya mnyama" # ni namba ya kibinadamu Maana zinazowezekana ni 1) namba inawakilisha mtu mmoja au 2) namba inawakilisha binadamu wote. # 666 "mia sita sitini na sita"