# Taarifa ya Jumla: Hii mistari ni mapumziko kutoka kwenye hesabu ya Yohana ya maono yake. Hapa anawaonya watu wanaosoma hesabu yake. # Ikiwa yeyote ana sikio Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asikilize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza" # Ikiwa yeyote amechukuliwa Usemi huu unamaanisha kuwa imashaamuliwa kuwa mtu atachukuliwa. Kama inahitajika, watafsiri wanaweza kusema dhahiri ni nani aliyeamua. "Kama Mungu ameamua mtu achukuliwe" au "Kama ni mapenzi ya Mungu kwamba mtu achukuliwe" # Ikiwa yeyote amechukuliwa mateka Nomino "mateka" inaweza kutajwa na kitenzi "kamata" "Kama ni mapenzi ya Mungu kwa adui kumkamata mtu fulani" # kwenye mateka ataenda Nomino "mateka" inaweza kutajwa na kitenzi "kamata" "adui atamkamata" # Ikiwa yeyote atauawa kwa upanga "Kama ni mpango wa Mungu kwa adui kumuua mtu fulani kwa upanga" # kwa upanga Upanga unaashiria vita. "vitani" # atauawa "adui atamuua" # Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu "Wale waliowatakatifu ni lazima wadumu katika uvumilivu na uwaminifu"