# aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele Huyu ni mtu mmoja. Yule ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi anaishi milele na milele. # milele na milele Maneno haya yana maana moja na yanarudiwa kuonesha msisitizo. "milele yote" # wazee ishirini na wanne wazee wanne -"wazee 24" # walisujudu wenyewe Kulala chini kwa kutazama ardhi. # kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi Hizi zilikua mfano wa taji za matawi ya mizeituni au majani ya laurusi yaliopondwa katika dhahabu. Mifano ambayo iliundwa kwa majani walipewa wanariadha washindi kuvaa kichwani. Wazee walikua wakionesha kuwa wanatii utawala wa Mungu. "walitupa chini mataji yao mbele ya kiti cha enzi kuonesha kumtii yeye" # Bwana wetu na Mungu wetu "Bwana wetu na Mungu." Huyu ni mtu mmoja yule ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi. # kupokea utukufu na heshima na nguvu Hivi ni vitu ambavyo Mungu anavyo siku zote. Kusifiwa kuwa navyo inazungumziwa kama kuvipokea. "kusifiwa kwa utukufu wake, heshima, na nguvu" au "kwa kila mmoja kumsifu kwa sababu yeye ni mtukufu, mwenye heshima, na mwenye nguvu.