# Taarifa ya Jumla: Yohana aanza kueleza maono yake ya kiti cha enzi cha Mungu. # Baada ya mambo haya "baada ya vitu ambavyo Yohana ametoka kuona" # mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni Msemo huu humaanisha uwezo ambao Mungu alimpa Yohana kuona mbinguni, angalau kwa njia ya maono. # ikizungumza nami kama tarumbeta Jinsi sauti ilikuwa kama tarumbeta inaweza kuainishwa vizuri. "kuzungumza na mimi kwa sauti kama sauti ya tarumbeta" # tarumbeta Hii humaanisha chombo cha kutengeneza muziki au kuwaita watu kwa ajili ya tangazo au mkutano. # nilikuwa katika Roho Yohana anazungumzia kuvutwa na Roho ya Mungu kana kwamba alikua katika Roho. "kushawishika na Roho" au "Roho alinishawishi" # yaspi na akiki Mawe ya thamani. Yaspi inawezekana ilikua nyeupe kama kioo # zumaridi Jiwe la thamani la kijani