# sinagogi la Shetani Watu wanaokusanyika kumtii au kumtukuza Shetani wanazungumziwa kama sinagogi, mahali pa wayahudi pa kuabudu na kufundishia. # kusujudu Hii ni ishara ya unyenyekevu, sio kuabudu. "Sujudu kwa unyenyekevu" # mbele ya miguu yako "mbele yako" # watajua "watajifunza" au "watakiri" # nitakulinda pia katika saa ya kujaribiwa "nitakutunza pia katika saa ya kujaribiwa" # saa ya kujaribiwa "muda wa kujaribiwa." Hii inaweza kumaanisha "wakati ambapo watu watajaribu kukufanya usinitii. # inakuja Iliyo siku za usoni inazungumziwa kama ijayo. # Naja upesi Inaeleweka kuwa anakuja ili ahukumu. "Ninakuja kuhukumu hivi punde" # Shikilia sana "Endelea kuamini" # taji Taji ilikua ni shada ambalo asili yake ilikua ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi ambayo yaliweka kwenye kichwa cha mwanariadha mshindi.