# yale uliyoyapokea na kusikia Hii humaanisha neno la Mungu ambalo waliamini. "neno la Mungu mlilosikia na ukweli mlioamini" # usipoamka Kuwa makina na hatari huzungumziwa kama kuamka. "Kuwa makini" au "Kuwa mwangalifu." # nitakuja kama mwivi Yesu atakuja wakati watu hawatarajii kama vile mwizi ajavyo asipotarajiwa. # majina machache ya watu Hii humaanisha watu wenyewe. "watu wachache" # hawakuchafua nguo zao Yesu anazungumzia dhambi katika maisha ya mtu kama vile ni nguo chafu. "hawajafanya maisha yao yawe yenye dhambi kama nguo chafu" # Watatembea pamoja nami Watu kawaida walizungumzia kuishi kama "kutembea." # wamevaa nguo nyeupe Nguo nyeupe huashiria maisha masafi bila dhambi. "na watavikwa nguo nyeupe ambayo inaonesha waso ni wasafi"