# Anapitisha hukumu "Anaamua mambo kwa usawa" # kwa waliokandamizwa "kwa watu waliokandamizwa" au "kwa wale ambao watu wengine wamewakandamiza" # kwa wenye njaa "kwa watu wenye njaa" au "kwa wale walio na njaa" # hufungua macho ya vipofu Kumsababisha mtu kipofu kuona inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa anafungua macho yake. "husababisha vipofu kuona" # vipofu "watu vipofu" au "wale walio vipofu" # Yahwe huwainua wale walioinama chini Yahwe kumsaidia mtu inazungumziwa kana kwamba anamsaidia mtu kimwili kusimama. "Yahwe huwasaidia wale walio kata tamaa" au "Yahwe huwasaidia wale walio wanyonge" # walioinama chini Hili ni tendo lenye ishara ya kukata tamaa na kuomboleza.