# Yahwe, mtu ni nini hadi unamtambua au mwanadamu hadi unamfikiria? "Mwanadamu ni mdogo sana ukilinganisha na vingine vyote ulivyoumba hadi ninashangaa kwamba unamtambua na kumwaza" # mtu ... mwanadamu maneno mawili yote yanamaanisha wanadamu # kama pumzi ... kama kivuli kipitacho Mwandishi anawafananisha wanadamu na hivi vitu kuonesha jinsi maisha yao yalivyo mafupi.