# Naitisha akilini "Nafikiria" # mafanikio yako "yote uliyotimiza" au "mambo yote makuu uliyotenda" # natawanya mikono yangu kwako katika maombi "naomba kwako na mikono yangu ikiwa imenyanyuka pembeni yangu" # nafsi yangu ina kiu na wewe katika nchi iliyokauka Mwandishi wa zaburi anazungumzia kutaka kuwa na Mungu kana kwamba yuko katika nchi iliyokauka na pia alikuwa karibu ya kufa kwa kiu. "ninataka kuwa na wewe kama mtu aliye katika nchi iliyokauka mwenye kiu sana anavyotaka maji" # nafsi yangu ina kiu na wewe Mwandishi anatamani kumjua Yahwe. Mkazo wa hamu yake kumjua yahwe ni kama mtu aliye na kiu sana. "na shauku na wewe" # nafsi yangu Nafsi ni njia nyingine ya kusema mtu. # nchi iliyokauka Ardhi ambayo kila kitu kimekufa kwa sababu hakuna maji. # Sela Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.