# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # umenichunguza "umenipima" # ninapoketi na ninapoinuka Mwandishi wa zaburi anatumia vitendo hivi viwili kuwakilisha kila kitu afanyacho. "kila kitu ninachofanya" au "kila kitu kunihusu mimi"