# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Nitakupa shukrani na moyo wangu wote Hapa moyo unawakilisha hisia. Kufanya kitu kwa dhati au kamili inazungumziwa kama kukifanya kwa moyo wote. "Nitakushukuru kwa dhati" # mbele ya miungu Maana zinazowezekana ni 1) "licha ya sanamu za uongo zilizopo" au 2) "mbele ya mkusanyiko wa mbinguni," ambayo inamaanisha "katika ufahamu wa malaika mbinguni" # Nitasujudu Kusujudu ni kitendo cha ishara kinachowakilisha kuabudu au kutoa heshima. "Nitakuabudu" # kutoa shukrani kwa jina lako "kukupa wewe shukrani" # neno lako Hii inamaanisha kile ambacho Mungu amesema. "kile ulichosema" au "amri zako na ahadi zako" # jina lako Maana zinazowezekana ni 1) "mwenyewe" au 2) "umaarufu wako"