# Makuhani wako wavikwe na uadilifu Uadilifu unazungumziwa kana kwamba ni nguo. "Watu watambue kuwa makuhani wako wana uadilifu" au "Nataka watu waone kuwa makuhani wako daima hufanya kilicho sawa" # Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi "Kwa sabau ya kilichotokea kwa mtumishi wako Daudi." # usigeuke kutoka kwa mfalme wake aliyetiwa mafuta Hapa "kugeuka" inamaanisha kumkataa mtu. "usimuache mfalme uliyemtia mafuta"