# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # wimbo wa upaaji Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi." # Wakulima wamelima mgongoni mwangu Mikwaruzo kutokana na kupigwa inazungumziwa kama kulima kwa mkulima. Mkulima alilima mistari yenye kina kirefu kiwanjani. "Adaui zangu wamenikata sana mgongoni mwanga" # wakaifanya mifuo yao kuwa mirefu Huu ni mwendelezo wa msemo wa ukulima. "Mfuo" ni mstari ambao mkulima aliulima. "walifanya mikwaruzo yao kuwa mirefu"