# Fanya wema, Yahwe Hili ni ombi. Nomino dhahania "wema" inaweza kuelezwa kama tendo. "Yahwe, tafadhali fanya vitu vizuri" au "Yahwe, nakusihi ufanye vitu vizuri" # walio sawa mioyoni mwao Hapa "mioyoni" inamaanisha hamu. "hamu ya kufanya kilicho sawa" # geukia Kukataa kumti Yahwe kunazungumziwa kama kugeuka kutoka njia nzuri. "acha kizuri na kwenda" # njia zao zilizopinda Hapa njia za uovu zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa ni njia ambayo haiko wima. "njia zao za uovu" # atawaongoza Watu wanaongozwa ili kuadhibiwa. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kuwaongoza ili kuwaadhibu"