# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # wimbo wa upaaji Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao watu waliimba walipokwenda Yerusalemu kusherehekea" au 2) "wimbo watu walioimba wakati wakipanda ngazi kwenda hekaluni" au 3) "wimbo ambao maneno yake ni kama ngazi." # Yerusalemu, miguu yetu inasimama ndani ya malango yako! Mwandishi anasitisha kuzungumza na wasikilizaji wake kwa muda na kuzungumza moja kwa moja na mji wa Yerusalemu. Yerusalemu inasemeshwa kana kwamba ni mtu anayeweza kusikia na kuandika. # miguu yetu inasimama Hapa "miguu" inamaanisha mtu mzima. "tunasimama" # ndani ya malango yako Hapa "malango" inamaanisha mji. "ndani yako, Yerusalemu"