# Taarifa ya Jumla: Hapa ni uhamisho kwenda katika hali ya mtu wa pili. Hii inaweza kumaanisha 1) mwandishi anaanza kuzungumza na wtu wa Israeli au 2) mwandishi anamnukuu mtu mwingine akizungumza na mwandishi. # mguu wako kuteleza Kuteleza kwa mguu kunahusishwa na kuanguka. "wewe kuanguka" # yeye anayekulinda ... mlinzi Misemo hii miwli inamaana kitu kimoja, na inasisitiza nafasi ya Mungu kama mlinzi. # yeye anayekulinda hatalala Hapa "kulala" inamaanisha kuacha kulinda. Hali yake hasi inaimarisha msemo. "Mungu hatalala na kuacha kuwalinda" au " Mungu atawalinda daima" # hatalala ... huwa halali wala kusinzia Misemo hii miwli inamaana sawa. Msemo wa pili unaimarisha wazo la kwanza. # Tazama Neno hili linatufanya kuzingatia kwa makini taarifa zinazofuata. # huwa halali wala kusinzia Mananeo haya mawili yana maana sawa. Hapa "kulala" inamaana kuacha kulinda. Hali yake hasi inaimarisha msemo. "hatalala na kuacha kuwalinda" au "atawalinda daima"