# RESHI Hili ni jina la herufi ya ishirini ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari wa msistari ya 153-160 unaanza na herufi hii. # Angalia mateso yangu Mwandishi wa zaburi anazungumzia mateso kana kwamba ni kitu ambacho watu wanaweza kuona. "Ona jinsi ninavyoteseka" # Tetea haja yangu "Nitetee dhidi ya wale wanao nishutumu" # niweke "linda maisha yangu" au "nipe uhai"