# ninayo hofu "ninaogopa sana" # hukumu zako za haki ni nzuri Mungu anahukumu kwa haki na maamuzi yake ni mema. "Hukumu yako ni ya haki na njema" # Tazama Hii ni lahaja. Hapa "Tazama" inamaanisha kuwa na ufahamu kuhusu jambo. Panapo lengwa ni maarifa na uelewa, na sio tu kutazama. # Nina shauku na maagizo yako Maana zinazowezekana ni 1) "Ninataka sana kujua maagizo yako" au 2) "Ninataka sana kutii kile unachotufundisha kufanya" # nifufue katika haki yako Neno "haki" ni nomino dhahania na inamaanisha kuwa mwenye haki. "nifufue kwa kuwa una haki" # nifufue Maana zinazowezekana ni 1) "Niweke kuwa hai" au 2) "Nifanye kuwa na nguvu"