# Geuza macho yangu yasitazame vitu visivyo na faida Hii ni sitiari inayomaanisha mtu anayetamani vitu ambavyo havina thamani ya milele. # nifufue katika njia zako "nifanye niweze kuishi kama unavyotaka niishi" # nifufue "fanya maisha yangu yawe imara" au "nipe nguvu" # Tekeleza kwa mtumishi wako ahadi yako uliyoahidi wale wanao kuheshimu "Fanya kwa mtumishi wako kile ulichoahidi kufanya kwa wale wanao kuheshimu" # mtumishi wako Mwandishi anajieleza kama mtumishi wa Mungu kuonesha unyenyekevu. "mimi, mtumishi wako"