# BETH Hili ni jina la herufi ya pili ya alfabeti ya Kihebrania. Katika lugha ya Kihebrabia, kila mstari katika mistari ya 9-16 unaanza na herufi hii. # Kijana atasafishaje njia yake? Swali hili linatumika kutambulisha faida mpya katika neno la Mungu. Swali hili balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hivi ndivyo kijana anavyoweza kusafisha njia yake" # atasafishaje njia zake Mwandishi anafananisha kuishi kulingana na sheria ya Mungu kama njia unayowekwa wazi bila vikwazo. # Kwa moyo wangu wote Hii ni lahaja. Moyo unawakilishi hisia, hamu, na mapenzi ya mtu. "kwa hali yangu yote" au "kwa kila kitu ndani yangu" au "kwa ukweli" # Usiniache nipotea kutoka katika amri zako Hapa kutotii amri za Mungu inaelezwa kama kupotoka njia. "Usiniache nikaidi amri zako"