# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # ALEFU Hili ni jina la herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kihebrania. # Wamebarikiwa wale "Ni vizuri vikoje kwa wale" # wale ambao njia zao hazina lawama Jinsi mtu anavyotenda inazungumziwa kama "njia." "wale ambao tabia zao hazina lawama" au "wale ambao hakuna anayeweza kuwalaumu kwa kutenda makosa" # wanao tembea katika sheria ya Yahwe Jinsi mtu anavyoishi au kutenda inazungumziwa kama kutembea. "wanaoishi kulingna na sheria ya Yahwe" au "wanaotii sheria ya Yahwe." Msemo huu unaweka wazi maana ya "ambao njia zao hazina lawama." # wanaomtafuta kwa moyo wao wote "Kumtafuta" Mungu inamaanisha kutaka kumjua. # kwa moyo wao wote Hii ni lahaja inayomaanisha kwa nguvu au kwa ukweli. "kwa hali yao yote" au "kwa kila kitu ndani yao" au "kwa kweli"