# Mataifa yote Hapa neno "mataifa" inawakilisha majeshi ya mataifa hayo. Mwandishi anatumi kukuza kwa neno kusisitiza idadi kubwa ya majeshi yaliyomzunguka. "Majeshi ya mataifa mengi" # katika jina la Yahwe Hapa neno "jina" linawakilisha nguvu ya Yahwe. "kwa nguvu ya Yahwe" # ninawakata Mwandishi anazungumzia kuyashinda majeshi ya adui kana kwamba alikuwa akiyakata kama mtu anavyokata tawi kwenye mmea. "niliwashinda" # wananizunguka kama nyuki Mwandishi analinganisha majeshi ya adui na kundi kubwa la nyuki yatamzunguka mtu" # walipotea haraka kama moto kwenye miiba Kama miiba iliyokauka inavyowaka upesi, mashambulizi ya majeshi ya adui yaliisha ghafla. "mashambulizi yao yalidumu kwa muda mfupi, kama moto unaoteketeza miiba unavyoisha upesi"