# Taarifa ya Jumla: Mtu aliyetunga zaburi hii anaendelea kuzungumza. # katika nchi ya walio hai "kwenye dunia hii ambapo watu wako hai." Hii ni tofauti na sehemu ya wafu. # Nimeumizwa sana Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ninahangaika sana" au "Watu wananiumiza sana" # Nikasema haraka "Nikasema haraka sana" au "Nikasema bila kutafakari" # Wanaume wote ni waongo "Kila mtu ni muongo" au "Watu wote ni waongo"