# Israeli, mtumainini Yahwe Neno "Israeli" linaashiria watu wa Israeli. "watu wa Israeli, mtumainini Yahwe" # msaada wenu na ngao Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni ngao kwa sababu anawalinda watu wake kama ngao inavyowalinda kutokana na madhara. "yule ambaye anawasaidia na kuwalinda" # Nyumba ya Haruni Hapa neno "nyumba" linamaanisha familia au uzao. Msemo huu unamaanisha makuhani, walikuwa uzao wa Haruni. "Uzao wa Haruni" au "Makuhani"