# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu Mwandishi anarudia msemo "sio kwetu" ili kusisitiza kwamba hawastahili kupokea heshima anayostahili Yahwe pekee. "Usilete heshima kwetu, Yahwe" # kwetu Neno "kwetu" linamaanisha watu wa Israeli. # lakini kwa jina lako leta utukufu Hapa neno "jina" linaashiria Yahwe mwenyewe. "lakini leta utukufu kwako mwenyewe" # kwa ajili ya uaminifu wako wa agano "kwa sababu ya uaminifu wako wa agano" # Kwa nini mataifa yaseme, "Yuko wapi Mungu wao?" Hili swali la balagha linasisitiza kuwa hakuna sababu ya mataifa kusema wanayosema. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Watu wa mataifa hawatakiwa kuwa na uwezo wa kusema, 'Yuko wapi Munguwao?'" # Yuko wapi Mungu wao? Watu wa mataifa mengine wanatumia swali hili kuwadhihaki watu wa Israeli na kuonesha kuwa hawaoni Yahwe akiwasaidia. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mungu wenu hayupo hapa kuwasaidia"