# Lakina ana... "Lakini Yahwe" # wahitaji Hii inamaanisha watu wahitaji. "watu wahitaji" au "watu maskini" # hujali familia zake kama kundi Hapa Daudi analinganisha jinsi Yahwe anavyowajali watu wake na jinsi mchungaji anavyojali kondoo wake. Maana zinazowezekana ni 1) "hufanya idadi ya watu kwatika famila zao kuongezeka kama kundi" au 2) "huwajali kama mchungaji anavyojali kondoo wake" # Wanyofu Hii inamaanisha watu wanaoishi maisha ya unyofu. "Watu wanyofu" au "Watu wanaofanya kilicho sawa" # uovu wote Hapa watu waovu wanazungumziwa kama "uovu." "watu wote waovu" # huziba mdomo hii inamaanisha kutokujibu kitu. "hana kitu cha kumjibu Yahwe" # ayaangalie mambo haya yote Hii namaanisha kuwaza vitu hivi. "kuwaza kuhusu hivi vitu" au "kukumbuka hivi vitu"