# Katika kambi Hii ina maana ya kambi ya Waisraeli katika nyika. "Katika kambi nyikani" # Dunia ilifunguka na kummeza Hapa jinsi ardhi inavyofunguka na kuwazika watu inalinganishwa kwa jinsi kiumbe kinavyomeza kitu. "Dunia ilifunguka na kuzika" # Dathani Huyu alikuwa afisa aliyeasi thidi ya Musa. # na kuwafunika wafuasi wa Abiramu Wafuasi wa Abiramu walizikwa pia dunia ilipofunguka na kumzika Dathani. "pia ikafunuka wafuasi wa Abiramu" au "na pia ikazika wafuasi wa Abiramu" # Abiramu Huyu alikuwa afisa aliyeasi dhidi Musa. # Moto ukaanza miongoni mwao; moto ukawateketeza waovu Misemo hii miwili ina maana kimoja na inaandikwa pamoja kusisitiza jinsi watu waovu waliuawa kwa moto.