# Aliwaokoa kutoka katika mkono ... na akawaokoa kutoka katika mkono Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inatumika pamoja kusisitiza ya kwamba Yahwe aliwaokoa kutoka kwa adui zao. # mkono wa wale ambao walimchukia Hapa "mkono" una maana ya uwezo na utawala. "uwezo wa wale ambao walimchukia" au "utawala wa wale ambao walimchukia" # yaliwafunika wapinzani wao Hii ni njia ya upole ya kuzungumza kuhusu yao kuzama majini. "alizamisha majini maadui zake" # Kisha wakaamini maneno yake Hapa nano "wakaamini" ina maana ya "mababu zao" na neno "yake" ina maana ya "Yahwe".