# Hufanya upepo kama wajumbe wake Maana zaweza kuwa 1) anasababisha upepo kuweza kubeba ujumbe kama mjumbe, "Hufanya upepo kuwa kama wajumbe wake" au 2) "Huwafanya wajumbe wake kuwa na haraka kama upepo" # miale ya moto watumishi wake Maana zaweza kuwa 1) "anasababisha miale ya moto kuwa kama watumishi wake". Husababisha moto kumtumikia kama mtumishi angefanya au 2) "hufanya mtumishi wake kuwa kama miale ya moto". # miale ya moto watumishi wake Hii inaweza kuandikwa na taarifa ya kudokezwa kutoka katika mstari wa nyuma. "Hufanya miale ya moto watumishi wake" # Alilaza misingi ya dunia Hapa msemo "kulaza misingi" ina maana ya "kuumbwa". "Aliumba dunia nzima"