# ni kutoka milele mpaka milele Hii ina maana ya kwamba upendo wa Yahwe huendelea milele. "utaendelea milele" # vizazi vyao "vizazi vya wale ambao humuinua yeye" # Wanashika agano lake na kukumbuka kutii maelekezo yake Misemo hii miwili ina maana za kufanana. # Yahwe ameimarisha kiti chake cha enzi katika mbingu Hapa utawala wa Yahwe kama mfalme unamaanishwa kama "kiti chake cha enzi". "Yahwe amechukua kiti chake katika mbingu ambapo hutawala kama mfalme" # ameimarisha "alifanya" # ufalme wake hutawala Hapa Yahwe anaelezwa kuwa "ufalme wake" kusisitiza mamlaka yake kama mfalme. "hutawala"