# Yahwe amekuwa mnara wangu wa juu Hapa "mnara" ni sitiari ya ulinzi. "Yahwe amenilinda dhidi ya adui zangu" # Mungu amekuwa mwamba wangu na ngome yangu Mwandishi anazungumzia Mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni sehemu ambayo mwandishi wa zaburi anaweza kwenda ili kuwa salama. "Nimemwomba Mungu kunilinda, na ameniweka salama kwa uwezo wake" # Atawaletea juu yao udhalimu wao wenyewe Maana zinazowezekana ni 1) "Atawafanyia vitu viovu walivyowafanyia wengine" au 2) "Atawaadhibu kwa matendo maovu yote aliyowatendea wengine." # atawakata Hii ni lahaja inayomaanisha "atawaua" # katika uovu wao wenyewe Maana zinazowezekana ni 1) "wakati wanafanya mambo maovu" au 2) "kwa sababu wamefanya mambo maovu."