# Taarifa ya Jumla: Mwandishi anatumia tashbihi kuelezea uharibifu kamili wa Mungu kwa adui wa Israeli. # wafanya kuwa kama mavumbi yanayozunguka, kama makapi mbele ya upepo Kauli zote mbili zinazungumzia Mungu kuangamiza adui zake kana kwamba alikuwa upepo mkali unaowapuliza kwa urahisi. # kama moto unaochoma msitu, na moto unaoweka milima katika moto Kauli zote mbili zinazungumzia adhabu ya Mungu kana kwamba ni moto, na adui wa Mungu ni vitu vinavyoungua katika moto. # Wafukuze kwa upepo wako wenye nguvu, na watishe kwa dhoruba yako Kauli zote mbili zinamwomba Mungu kuangamiza adui kwa dhoruba.