# Taarifa ya Jumla: Misemo hii miwili yote ina maana za kufanana na inaunganishwa kwa ajili ya kuweka mkazo. # Mwaga gadhabu yako kwa mataifa Asafu anazungumzia gadhabu ya Mungu kana kwamba ilikuwa ni kimiminiko. "Kwa kuwa una hasira, adhibu mataifa" # haliiti jina lako Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema nguvu na mamlaka ya mtu. "sio wako" au "hawakuombi wewe kuwasaidia" # wamemmeza Yakobo Neno "Yakobo" ni njia nyingine ya kusema uzao wako, watu wa Israeli. "wamewaangamiza kabisa watu wa Israeli"