# Taarifa ya Jumla Mwandishi anaendelea kuelezea kile ambacho Mungu alifanya kwa watu wa Israeli. # mkono wake wa kuume ulipata Maneno "mkono wa kuume" ni njia nyingine ya kusema uweso. "alijishindia kwa kutumia uwezo wake mwenyewe" # akawagawia urithi wao Maana zinazowezekana ni 1) Mungu aliwapangia Waisraeli urithi wao katika nchi ambayo mataifa mengine yaliwahi kuishi au 2) Mungu aliyapangia mataifa aliyoyaondoa urithi sehemu nyingine. "aliwapa nchi ambayo itakuwa yao daima" # katika mahema yao Maana zinazowezekana ni 1) aliweka Israeli katika mahema yao wenyewekatika nchi au 2) aliwaweka Israeli katika mahema ambamo aliwaondoa mataifa mengine. "Mahema" mengi haya yalikuwa nyumba kabisa, wakati mataifa mengine yalipoishimo na Waisraeli walipoishimo.