# nilinyosha mikono yangu "niliomba na mikono yangu ikiwa imenyoshwa" # Nafsi yangu ilikataa kufarijiwa "Nafsi" ni njia nyingine ya kusema mtu. "Sikumruhusu yeyote kujaribu kunifariji" # Nilimuwaza Mungu na nikagumia; Nilimuwaza huku nikiishiwa nguvu Misemo hii miwili ina maana za kufanana na inaunganishwa kwa ajili ya mkazo. # huku nikiishiwa nguvu "wakati nafsi yangu ikiishiwa nguvu" au "wakati nafsi yangu ilipolemewa" # Sela Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kiebrania, na zingine haziliweki.