# Taarifa ya Jumla: Asafu anamzungumzia Mungu. # huleta chini na huinua juu "huwashusha watu wengine na kuwainua watu wengine." Maneno "huleta chini" na "huinua juu" ni sitiari ya Mungu kuwapa nguvu watu na kuchukua nguvu yao. "humfanya mtu mmoja mfalme katika nafasi ya mwingine" au "huondoa nguvu ya mtu mmoja na kumpa nguvu mtu mwingine" # kikombe cha divai ya povu ... imechanganywa na vikolezo Yahwe anapowaadhibu watu watakuwa kama watu waliokunywa divai kali na kuugua. # divai ya povu Povu ni sitiari ya nguvu ya divai kuwafanya watu walewe. "divai kali" # vikolezo majani yaliyo kaushwa au mbegu za ardhini # kuimwaga nje kuimwaga kutoka kwenye chombo kikubwa hadi kwenye vikombe ambavyo watu watatumia kunywa # watainya hadi tone la mwisho "kunywa kila tone lake"