# Taarifa ya Jumla: Asafu anaendela kuomboleza kwa Yahwe. # sehemu zenye giza za nchi zimejaa sehemu za vurugu Asafu anazungumzia "sehemu" kana kwamba ni chombo ambamo mtu anaweza kuweka "sehemu za vurugu." "watu wenye vurugu wanafanya matendo maovu katika sehemu za giza nchini pale wanapoweza" # sehemu zenye giza za nchi Neno "giza" linaweza kuwa ni sitiari ya sehemu ambapo mambo mabaya yanatokea au nchi ambazo Waisraeli walipelekwa katika uhamisho. # Usiwaache walio kandamizwa warudi na aibu "Usiwaache watu waovu wawashinde walio kandamizwa na kuwaaibisha" # walio kandamizwa Hawa ni watu wanaotendewa ukatili na watu wenye nguvu. # maskini na walio kandamizwa Maneno "maskini" na "walio kandamizwa" yanamaanisha kitu kimoja na yanasisitiza kuwa Yahwe anawaokoa wengi wanaohitaji msaada wake.