# Taarifa ya Jumla: Asafu anaendelea kueleza ambavyo wakati mwingine anataka kulalamika kwa Mungu kuhusu wale ambao wana "kiburi" na "waovu" # watu wake wanawageukia Maana zinazowezekana ni 1) "Watu wa Mungu wanawapenda watu waovu" au "watu waovu wanarudi sehemu hii" # maji mengi yanatolewa Maana zinazowezekana ni 1) "Watu wa Mungu wanasikiliza kwa furaha maneno ya watu waovu" au 2) "watu waovu wana chakula cha kutosha kula na divai ya kunywa" # Wanasema watu waovu wanasema # Mungu anajuaje? Kuna ufahamu kwa Aliye juu? Maswali haya yenye balagha yanaonesha dharau kwa Mungu. Maswali haya yanaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakika Mungu hajui tunalolifanya. Aliye juu hana ufahamu wa hili."