# zaidi na zaidi "zaidi wakati wote" au "daima zaidi ya nilivyofanya kabla" # Mdomo wangu utaeleza Mdomo ni njia nyingine ya kumwakilisha mtu mzima. "Nitaeleza" au "Nitazungumza kwa mdomo wangu na kueleza" # haki yako "jinsi ulivyo mwenye haki" au "vitu vyote vizuri unavyovifanya" # wokovu wako "jinsi ulivyoniokoa" au "jinsi unavyookoa watu" # ingawa "hata kama" # Nitakuja Maana zinazowezekana ni 1) "Nitaenda mahali ambapo watu wanamwabudu Yahwe" au 2) "Nitaenda kwa adui zangu" # kwa matendo makuu ya Bwana Yahwe Maana zinazowezekana ni 1) "nitawaambia kuhusu matendo makuu aliyoyafanya Bwana Yahwe" au 2) "kwa sababu Bwana Yahwe amenipa nguvu kufanya matendo makuu" # nita taja "nitazungumzia"