# Wapole Hii inamaanisha watu wapole kwa ujumla. "Watu wapole" # nyie mnaomtafuta Mungu Kumtafuta Mungu inawakilisha kati ya 1) kumwomba Mungu msaada au 2) kumuwaza Mungu na kumtii. "nyie mnaomwomba Mungu msaada" au "nyie mnaomuwaza Mungu" # acha mioyo yenu iishi Hapa "mioyo" inamaanisha watu. Hapa "kuishi" ni lahaja inayomaanisha kutiwa moyo. "na utiwe moyo" # Yahwe huwasikia Hapa "huwasikia" inamaanisha hujibu. "Yahwe hujibu" # wahitaji Hii inamaanisha watu wahitaji kwa ujumla. "watu wahitaji" # wafungwa wake "wale walioteseka kwa ajili yake"